Wednesday, September 14, 2011

JUMLA YA MAITI 202 ZIMEPATIKANA KATIKA AJARI YA MELI YA Mv.Spice Islander.

0 comments
Tangu zoezi la uwokoaji limeanza Jumla ya maiti 202 tayari zimepatikana katika ajali ya Meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea hivi karibuni huko Nungwi Zanzibar.


Maiti tano zaidi zilipatikana hapo jana sehemu ya Mwambao shimoni Mombasa Kenya ambapo maiti zote hizo zilizikwa huko huko Kenya kutokana na hali ya maiti hao zilivyokuwa ambapo kabla ya jana maiti 197 zilikuwa zimepatikana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed zilieleza kuwa aliwasiliana na Balozi mdogo wa Tanzania Nchini Kenya na kumthibitishia kwamba isingewezekana kuwasafirisha maiti hao kuwaleta Zanzibar kwa ajili ya kutambuliwa na jamaa zao kutokana na hali ilivyokuwa.

Amesema maiti hao mmoja inakadiriwa ni miaka minane, mwengine miaka 20 hadi 25 na wengine miaka 40 wote ni wanaume na mtoto mchanga mwanamke anakadiriwa na umri wa mwaka mmoja na nusu ambao wamepatikana katika kijiji cha Diani.

Kazi ya uokoaji bado inaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa vikosi vya ulinzi na usalama, raia wa Tanzania pamoja na kikosi maalum cha Uokozi kutoka Afrika ya Kusini.

Wakati huo huo michango ya Rambi rambi inaendelea ambapo hapo jana Isnaashir imetoa jumla ya Shl. Milion 30, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wametoa shl.Milion 15 Wabunge wa Afrika Mashariki wamechangia sh.Milion 2 na Benki ya NMB imekabidhi hundi ya sh.Milion 20.

Fedha zote hizo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maafa ya kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Shughuli za uchangiaji bado zinaendelea na wananchi pamoja na Taasisi mabalimbali za binafsi na Serikali zinaendelea kutoa michango yao.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KUMBUKUMBU YA MIAKA 35 YA RELI YA TAZARA.

0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.

baada ya hutuba hiyo makamu wa rais alipata fulsa ya kusikiliza maelekezo kutoka kwa meneja wa Tazara, ndugu Mkandarasi Abdallah Shekimweri wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara pia alipata fulsa ya kutembelea moja ya mfumo wa Behewa Daraja la kwanza Treni ya Tazara
Mwisho kabisa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhi zawadi kwa wageni wakiwemo aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Job Lusimbe pamoja na (mzee John Nchimbi na mkewe, Sylviaa Nchimbi) waliokuwa abiria wa kwanza kusafiri na reli ya Tazara mwaka 1976,ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika ujenzi wa reli ya Tazara.

WATANZANIA WATAKIWA KUNUNUA BIDHAA ZENYE NEMBO YA TABAKA LA OZONI.

0 comments
Watanzania wametakiwa kununua bidhaa zenye nembo ya tabaka la hewa ya Ozoni (Ozone rafiki) ili kuungana na mataifa mbalimbali duniani kuhifadhi tabaka la hewa hiyo ambalo liko hatarini kutoweka angani kutokana na uchafuzi wa mazingira unaoendelea sasa duniani kote.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yatakayofanyika kitaifa mwezi huu Mjini Arusha, kaimu mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Stephen Nkondakaya amesema kuwa licha ya Tanzania kukabiliwa na changamoto mbalimbali inaendeleza jitihada mbalimbali za kupunguza ongezeko la matumizi ya vifaa vinavyo haribu tabaka la Ozoni angani.

Amesema hali iliyoanza kujitokeza ya kuruhusu kiasi kikubwa cha mionzi ya kikiukaurujuani kufika kwenye uso wa dunia inasabishwa na matumizi ya kemikali hatari zikiwemo “Chlorofluorocarbons”,Halons na Carbon tetrachlorides zinazotumika katika sehemu mbalimbali zikiwemo kwenye majokofu, viyoyozi , vifaa vya kuzimia moto, shughuli za usafishaji vyuma aina zote, utengenezaji wa magodoro, kilimo cha tumbaku na maua zimekuwa chanzo cha uharibifu wa tabaka la Ozoni.

Bw. Nkondokaya amefafanua kuwa hali ya kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi , uharibifu wa macho unaosababisha upofu, upungufu wa kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi kuathirika kwa maumbile na michakato ya ukuaji kunasababishwa na ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabia nchi.

Ameeleza kuwa Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 198 zilizoridhia mkataba wa kimataifa wa Vienna na Itifaki ya Montreal mwaka 1993 inaendelea kuweka mfumo wa udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ikiwemo kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku na vifaa vinavyotumia gesi hizo kama vile majokofu na viyoyozi vilivyokwisha tumika na vinavyotumia vipoozi aina ya R 11 na R 12,kuepuka kutupa ovyo majokofu ya zamani na vifaa vya kuzimia moto vinavyoharibu tabaka la Ozoni aina ya CFCs na halon.

Kuhusu maadhimisho ya Kimataifa ya Tabaka la Ozoni ambayo kitaifa yatakayofanyika Mjini Arusha amesema yataongozwa na kauli mbiu ya “Uondoshaji wa Matumizi ya gesi za “Hydrochrolofluorocarbons”: Mchango muhimu katika kulinda Tabaka la Ozoni na kuzuia Mabadiliko ya Tabianchi” na kuambatana na zoezi la utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulinda tabaka la Ozoni pamoja na kugawa mitambo ya kutambua gesi zinazoharibu tabaka la hewa ya Ozoni kwa wadau wa usimamizi wa sheria ya mazingira nchini.

Sunday, September 11, 2011

Ko Koe f. DJ Paul & Glasses Malone - "Every Day In My Hood"

0 comments

Tech N9ne - Beautiful Music Feat. Krizz Kaliko [Welcome To Strangeland]

0 comments

Ace Hood - "Letter To My Exs" / "Tear Da Roof Off"

0 comments

Ace Hood release his second set of Blood sweat and Tears video.

Freddie Gibbs Ft Insanity-U Know What To Do

0 comments
Freddie Gibbs has been release new hits.

Drake Feat. Rick Ross - Free Spirit (Take Care)

0 comments

Rapper Drake contunue to release single continuously special for his fans to continue enjoy his work.

Waka Flocka Feat. Drake - Round Of Applause (Remix) 2011

0 comments

Drake adds verse to walk flackas Round of Applause single.

Drake "Club Paradise" [TAKE CARE]

0 comments

Drake release another for the night, it’s called “Club Paradise”.

Tyga-Far Away ft Chris Richardson

0 comments

watch out New video Far Away from Tyga.

Saturday, September 10, 2011

Big sean "Marvin & Chardonnay"featuring kanye west & Roscoe Dash

0 comments

Music video from Big sean for his single "Marvin & Chardonnay"featuring kanye west & Roscoe Dash.The track was produced by No I.D and the video was directed by Hyper williams.

Emilio Rojas-Breaking Point

0 comments
video for the single from Emilio Rojas 'upcoming project'.

Lloyd - Saturday Night

0 comments

Young Jeezy ft. Freddie Gibbs - Nicks 2 Bricks

0 comments
Rapper Young-Jeez has release new song called Nicks 2 Brick.
 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |