Monday, November 14, 2011

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UBIA KATIKA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVRNMENT PARTNERSHIP)

0 comments
MATHIAS CHIKAWE (MB.)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS–UTAWALA BORA
Ndugu zangu wanahabari, nimewaita ili nizungumze nanyi juu ya Mpango wa Ubia katika Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi (Open Government Partnership - OGP).

Mpango huu ambao ni juhudi mpya za kimataifa katika kuendesha Serikali kwa uwazi na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, ulizinduliwa rasmi na Viongozi wa nchi za Marekani, Brazil, Indonesia, Mexico, Norway, Philippines, Afrika ya Kusini na Uingereza mnamo tarehe 20 Septemba 2010 wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.

Nchi hizi waanzilishi kwa pamoja zilipitisha Azimio la kuendesha Serikali kwa uwazi na uwajibikaji kwa kuweka bayana Mipango ya utekelezaji katika nchi zao.

Kwa kutambua umuhimu wa mpango huu, Tanzania imeridhia kujiunga na mpango huo. Hadi sasa nchi nyingine 37 zimeridhia kujiunga na mpango huo zikiwemo nchi nyingine nne kutoka Bara la Afrika ambazo ni Afrika ya Kusini, Ghana, Kenya na Liberia.

Ndugu wanahabari, msisitizo mkubwa wa mpango huu ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Serikali, kuwawezesha wananchi kupata taarifa sahihi na kuzitumia kwa maendeleo yao, kuzuia na kupambana na rushwa na kusisitiza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika kuimarisha utawala bora.

Ili kuwa mwanachama wa mpango huo, nchi zinatakiwa kuunga mkono Azimio la Uwazi katika Kuendesha Serikali; kuandaa Mpango Kazi kwa kushirikiana na wananchi na kuweka utaratibu wa uwazi wa kutoa taarifa za utekelezaji wa mpango kazi huo.

Ndugu wanahabari, hatua ya kwanza ya kuchukua baada ya nchi kuridhia kujiunga na mpango huo muhimu ni kuandaa mpango kazi unaoshirikisha wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia, Sekta Binafsi na Umma kwa ujumla.

Mpango huu unatakiwa kuandaliwa kwa uwazi, na kwa kuanzia utahusisha vipaumbele vichache vitakavyotekelezeka. Mpango utaendelea kuongeza maeneo mengine ya utekelezaji kadri uzoefu utakavyopatikana.

Vipaumbele vya awali vitahusu kuimarisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwenye sekta tatu za Afya, Elimu na Maji.

Napenda kupitia kwenu kuwataarifu Watanzania wote kwamba, Serikali imeanza rasmi mchakato shirikishi wa kuandaa Mpango Kazi wa Uwazi katika kuendesha shughuli za Serikali. Maandalizi ya mpango huu yatashirikisha wadau niliowataja awali, na tutatumia njia mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kutoa maoni yao kuhusu maeneo mahsusi ambayo yakiboreshwa, utoaji wa huduma utaimarika.

Kutakuwa na mikutano ya wazi ambapo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla watapata fursa ya kujadiliana na Serikali ili kupata mwafaka wa pamoja wa yale ambayo yatawekwa kwenye mpango unaoandaliwa.

Aidha, Tovuti ya www.mwananchi.go.tz, barua za kawaida kupitia posta (Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam), ujumbe kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua pepe: ogp@ikulu.go.tz na blogu: www.ogptz.com zitatumika kukusanya maoni ya wananchi. Mawazo yote yatakayotolewa yatafanyiwa kazi na kwa uwazi mkubwa.

Ndugu wanahabari, rasimu ya mpango unaoandaliwa itajadiliwa katika kikao cha Mawaziri wa nchi zinazohusika na mpango huu. Kikao hicho kitafanyika tarehe 7 – 8 Desemba, 2011 huko Brasilia - Brazil.

Katika kikao hicho, nchi zitabadilishana uzoefu wa maandalizi ya mipango kazi ili hatimaye kuwa na rasimu itakayowasilishwa kwenye kikao cha Wakuu wa Nchi wanachama kitakachofanyika Brazil, mwezi Machi 2012. Baada ya Mpango huu kupitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi, kila nchi mwanachma itaanza utekelezaji.

Napenda niwakaribishe kwa dhati kabisa Wananchi kushiriki kutoa maoni yenu yatakayosaidia kuandaa mpango wa kitaifa wa kuongeza uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika utendaji wa kazi za Serikali. Waandishi wa habari mna dhamana na wajibu mkubwa wa kuelimisha umma kushiriki kutoa maoni yao ili mpango unaoandaliwa ukamilike kwa wakati.

Hatuna muda mrefu sana kati ya sasa na tarehe ya kukamilisha rasimu ya kwanza ya mpango huo ambayo ni tarehe 7 Desemba, 2011. Nina imani kwa kushirikiana kipindi hiki kinatosha kukamilisha kazi hii. Ni vyema vyombo vyote vya habari vikaubeba ujumbe huu mzuri na kuufikisha kwa wananchi kwa nia ya kuwaelimisha na kuwahamasisha kushiriki kutoa maoni.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza!

MATHIAS CHIKAWE (MB)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS–UTAWALA BORA
IKULU
DAR ES SALAAM.
Tarehe 14 NOVEMBA, 2011

MKUTANO WA UBORESHAJI WA MAZAO YA UVUVI NA MPUNGA KWA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI WAFUNGULIWA LEO JIJINI DAR

0 comments
Naibu Katibu Mkuu Wizara Kilimo Chakula na Ushirika,Mhandisi Mbogo Futakamba akifungua mkutano unaojadili uboreshaji wa mazao ya uvuvi na mpunga kwa ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku tano unalenga kuwawezesha wakulima kuzalisha mpunga kwa wingi huku wakiendeleza ufugaji wa samaki katika maeneo yao ya kilimo ili kupunguza umaskini.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.

UJENZI WA DARAJA KATIKA KIJIJI CHA MATAI WILAYANI SUMBAWANGA.

0 comments
Wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya kichina iitwayo China Railway 15Bureuau Group Corporation (CR 15G) Newcentry Company Limited wakijenga daraja katika kijiji cha Matai wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa hivi karibuni katika barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga inayotengenezwa kwa kiwango cha lami na kampuni hiyo ya ujenzi hata hivyo kazi katika barabara ni za kusua kusua kufuatia Serikali kushindwa kuwa lipa wakandarasi hao malipo yao kwa wakati.

PUSH OBSERVER YAPATA CEO MPYA

0 comments
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI inayoongoza ya usimamizi wa vyombo vya habari katika nchi za Afrika Mashariki, Push Observer imemtangaza gwiji la sekta hiyo Duniani, Joe Taylor kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wake.

Akizungumza jijini leo, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Push Observer, Omari Salisbury alisema kuwa hatua ya kumwajiri Taylor imetokana na historia yake nzuri katika sekta hiyo nchini Marekani na kampuni yao inataka mafanikio makubwa katika sekta hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Salisbury alisema kuwa Taylor ambaye kwa sasa amekwisha anza kazi, alikuja nchini kwa mara ya kwanza mwezi Septemba na kuendesha ‘semina’ kwa wadau mbali mbali kwenye hotel ya Sea Cliff na kuwafumbua macho wadau wengi wa sekta hiyo.

Alisema kuwa wanaamini kuwa ujio wake na kufanya kazi na kampuni hiyo kutawawezesha kupata maendeleo makubwa huku wakitoa huduma bora zaidi katika Nchi za Afrika Mashariki.

“Lengo ni kupata maendeleo makubwa katika sekta ya usimamizi wa habari, tumeamua kuajiri mtu bora kabisa kwa lengo la kutoa huduma bora kabisa, naamini wadau wetu wakiwemo waandishi wa habari watapata kile wanachokihitaji katika kazi zao,” alisema Salisbury.

Alisema kuwa Taylor ni kiongozi bora na amekuwa katika fani hiyo kwa miaka 30 nchini Marekani. Kabla ya kujiunga na Push Observer, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya VMS na mwaka 2009 walifanikiwa kushinda tuzo ya mwaka ya Innovation (Innovation of the Year Award) na mwaka huo huo wakashinda tuzo ya Cost Saving Award.

Talylor vile vile amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ikiwa pamoja na makamu wa Rais wa kampuni ya Broadcast Monitoring for Medalink na Rais wa Broadcast News Mid-America, Oklahoma.

Taylor alisema kuwa amefurahi kujiunga na Push Observer na kufanya kazi Tanzania na anaamini kuwa kampuni hiyo itafika mbali kwa kupata maendeleo makubwa.

WASHINDI WA REDDS UNI FASHION BASH JIJINI MWANZA WAPATIKANA

0 comments
Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Buttalah akimkabidhi mshindi wa kwanza wa Ubunifu toka chuo kikuu cha SAUT Bwana Simon Joseph Kiasi cha 700,000 alipoibuka mshindi kwenye Redds Uni Fashion Bash mkoa wa Mwanza.
Mwakilishi wa TBL Mkoani Mwanza akimkabidhi zawadi ya Tsh 500,000 mshindi wa kwanza wa upande wa mitindo,Oliver Kikare baada ya kuibuka mshindi kwenye fainali za Redds Uni Fashion Bash Mkoa wa Mwanza, Anasoma Chuo kikuu cha SAUT
Washiriki upande wa mitindo kwenye Redds Uni Fashion Bash wakipita kwa pamoja jukwaani kabla ya kutangazwa kwa washindi,hapa walikuwa wakionyesha mavazi maalum kwaajili ya muda tofauti tofauti wa mchana na usiku.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Mwana Fa akifanya vitu vyake kwenye Tamasha hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa M10 kwenye chuo kikuu cha Saint Augustino jijini Mwanza usiku wa jana.
Majaji wa tamasha hilo,Costantine Magavile na Mr Tanzania walishiriki kwa pamoja kumtafuta mwana mitindo na mbunifu wa Redds Uni Fashion Bash jijini Mwanza wakitazama kwa umakini washiriki wakati walipokuwa wakipita jukwaani, nyuma yao ni wanavyuo wakishangilia katika moja ya matukio ya washiriki.
Meneja masoko wa TBL,Fimbo Buttalah (pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wa TBL wakifuatilia kwa ukaribu mashindano hayo.

THE SWAHILI CENTER REPRESENTS LOCAL STAKEHOLDERS AT CULTURE FORUM IN GHANA

0 comments
Kheri Jumbe (left) speak about the status of the culture and creative industry in Zanzibar. On the panel are delegates from Angola, Accra, Nigeria and Rwanda.

The Swahili Performing Arts Center Managing Director, Kheiri Jumbe, will this week be attending the African Cultural Capital’s City Forum on Culture and Development in Accra, Ghana. The aim of the City Forum on Culture and Development is to strategize on ways to infuse Culture and creative industry agendas at the heart national development policy agendas.

During the forum, culture leaders from several African countries will explore development policies in their respective countries in relation to funding modalities and programming approaches . Countries represented at the forum taking place from 7-10 November 2011 are the hosts Ghana, Tanzania, Cameroun, Morocco, South Africa, Nigeria and Mozambique. Delegates taking part in the forum include cultural leaders, Parliamentarians, civic officials and members on several international agencies dealing with culture and the arts.

The Mayor of Accra, Hon. Alfred Oko Vanderpuije, will be the host of the 4-day event which has been organized by the City of Accra, The Arterial Network, UNESCO, The Goethe Institut and Agenda 21 of Spain.

‘My personal ambition and that of the Swahili Center as stakeholders in culture in Tanzania is to develop ways in which the competitiveness of culture in the context of its productivity can be enhanced for the benefit of the local economy,’ commented Mr. Jumbe when asked about the purpose of his participation.

Many studies conducted on the social and economic impact of cultural and creative industries have shown positive contribution towards social cohesion, economic development and poverty reduction. UNCTAD data shows that cultural and creative industries worldwide grew an average of 8.7% annually.

However, in many developing countries culture is not mainstreamed into development policies despite UNESCO recognizing it as a vector for development and promoter of international cooperation. As a result, there is generally lack of long-term, coordinated effort and funding in the sector in many developing countries.

Inevitably, most support for culture in developing countries comes from international donors and multinational corporations, who only tend to concentrate on short-term and highly visible projects that are usually insufficient to render the sector viable.

Zanzibar has been invited to participate at the forum on the merit of both the tangible and intangible cultural assets present in Stonetown. The Forum is taking place at the renowned Accra International Conference Center.

The Swahili Performing Arts Center is a local not-for-profit organization based in Zanzibar and operates under the mission of furthering the development of authentic Swahili performing arts disciplines from Zanzibar and the Swahili Coast through empowerment, production, presentation and outreach.

TAIFA STARS WAREJEA NCHINI NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE

0 comments
Wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania ‘taifa stars’ wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo wakitokea N’Djamena ambapo waliifunga timu ya taifa ya Chad kwa mabao 2-1. Timu hizo zinarudiana kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars,Jan Paulsen akiongea na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Taifa Stars wamewasili leo wakitokea N’Djamena nchini Chad kushiriki mchezo wa kimataifa ambapo waliifunga timu ya taifa ya Chad kwa mabao 2-1.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakiwa ndani ya Basi lao.
Washabiki wa wakiwa wameizunguka Basi iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Timu ya Taifa.

MNH RECEIVES THE WORLD QUALITY COMMITMENT AWARD GOLD CATEGORY

0 comments
World Quality Commitment Gold Trophy Awarded to MNH recently in Paris
From Left: Mr. Makwaia Makani the then Acting Executive Director of MNH receiving the trophy from President and CEO of B.I.D. Mr. Jose E. Prieto (centre) in Paris, along with Dr. Hedwiga Swai, Acting Director of Medical Services.
Muhimbili National Hospital has received the World Quality Commitment Award gold category in recognition of its commitment to quality of services, leadership, and utilization of technology, innovations and customer satisfaction.

The World Quality Commitment Convention and presentation of the 2011 International Quality Awards took place recently in Paris at the Concorde La Fayette Hotel.

The World Quality Commitment Award is presented to outstanding companies as an entity for corporate achievement to recognize leadership, quality of services offered by individual companies to its clients, use of technology,customer satisfaction and prestige of organizations in different countries throughout the world; that further their reputation and position by implementing and promoting quality culture. MNH has complied with these set standards.

This award is coordinated by Business Initiative Directions (B.I.D) based in Paris.

The voting process was carried out during the B.I.D World Congress with meetings in Paris, London, Geneva,Frankfurt, Madrid and New York over the past ten years based on one or several of the following concepts;The Quality Commitment QC100 principles, Customer Satisfaction, Leadership, Technology, Best Practice,Business Results, ISO 9000 and TQM.

Describing the Award, the President and CEO of B.I.D. Mr. Jose E. Prieto said that the awarded organizations are symbols of commitment to leadership, technology and innovation, making them models for others in their sectors.

According to Mr. Makwaia Makani, then Acting Executive Director, who was in Paris to receive the Award on behalf of the Hospital along with Dr. Hedwiga Swai, Acting Director of Medical Services said the award will stimulate the Hospital commitment to quality service delivery.

Muhimbili National Hospital has received a certificate and a gold trophy in recognition of this achievement.

The Hospital further commits itself to continued quality health care delivery to the nation.

MTAALAMU WA KUIGIZA SAUTI ZA WATU

0 comments

DEREVA WA BODABODA AUWAWA NA KUNYOFOLEWA MACHO JIJINI ARUSHA

0 comments
Na Gladness Mushi - Arusha

Mwili wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni dereva wa bodaboda, ambaye hakutambulika kwa haraka,umekutwa umetelekezwa kandokando ya Mto kwenye shamba la migomba, ukiwa na majeraha kichwani na macho yakiwa yamenyofolewa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Akili Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema tukio la kukutwa kwa mwili huo limetokea novemba 8 mwaka huu majira ya saa12 jioni katika mtaa wa jamuhuri daraja mbili katika manispaa ya Arusha.

Alisema kuwa marehemu alikutwa katika shamba la migomba ambalo linamilikiwa na Richard Laiza ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo.

Alifafanua kuwa Laize ndiye aliyeuona mwili huo na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa huo Husseini Dudu,ambaye baada ya kushuhudia tukio hilo aliyoa taarifa polisi.

Aidha uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kwamba marehemu alipigwa na kitu kizito na chenye ncha kali kichwani na kisha kutelekezwa katika shamba hilo.

Hata hivyo kwa kuwa mwili huo ulibainika kuharibika vibaya na uchunguzi wa daktari ulifanyika eneo hilo la tukio na mwili wa marehemu ulizikwa katika shamba hilo baada ya kutofahamika ndugu wa marahamu huyo.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wa mauaji hayo.

MICHUANO YA KIMATAIFA MPIRA WA WAVU KOMBE LA NYERERE KUFANYIKA MJINI MOSHI

0 comments
Si rahisi kumtenganisha baba wa Taifa mwalimu Julius K. Nyerere na uhuru wa nchi yetu. Kwa kulitambua hilo TAVA inasherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwa aina yake kwa kumkumbuka Baba wa taifa katika kipindi cha sherehe za miaka 50 ya uhuru. TAVA inaandaa shindano la kimataifa linalojulikana kama "MICHUANO YA KIMATAIFA MPIRA WA WAVU KOMBE LA NYERERE" litakalofanyika mjini moshi katika viwanja vya hindumandal kuanzia tarehe 5 mpaka 9 Dec siku ya kilele cha sherehe za uhuru.

Michuano hii inashirikisha vilabu vya wanaume na wanawake kutoka katika nchi jirani za Afrika mashariki. Tunategemea timu kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na pia kutoka Zambia, ambapo tayari wamesha patiwa mialiko na kuonyesha nia ya kushiriki.

Timu wenyeji za wanaume na wanawake zitakazo shiriki ni Jeshi stars, Magereza, JKT za Dar, Mzinga ya Morogoro, Polisi Tz, Mafunzo na Nyuki za ZNZ, Kijichi ya Dar, Makongo na lord baden sec schools, Timu za vyuo vikuu vya Moshi KCMC na MUCCoBS, Arusha Volleyball club (AVC), Tanga central na Rukwa Volleyball club.

TAVA inachukua nafasi hii kutafuta wadhamini kujitokeza kudhamini mashindano hayo makubwa kuwahi kufanyika katika historia ya mpira wa wavu nchini kwani ni maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru tukisheherekea na nchi jirani katika michezo.

Nashukuru sana na kwa mawasiliano zaidi:-
Alfred Selengia,
M/kiti - kamati ya maendeleo ya mpira wa wavu - TAVA
0655 710302

Katibu Mkuu wa TAVA
Allen Alex
0713 550798

Sunday, November 13, 2011

MKUU WA MKOA WA MOROGORO ATEMBELEA SEHEMU ILIYOTOKEA AJALI LA LORI

0 comments
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto) akifuatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Baruani, wakiliangalia lori lililoanguka juzi usiku katika barabara ya Morogoro- Dodoma na kwa mbali ni Mkuu wa Mkoa huyo akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa Lori hilo lenye namba za usajili T 838 BTY na Tella namba T 215 BTE.



INVESTIMENT'S OF BULYANHULU GOLD MINE IN EDUCATION, HEALTH PROJECTS.

0 comments
AFRICAN Barrick Gold's (ABG) Bulyanhulu Gold Mine has this month spent close to 150 million/- on key education and health projects expected to benefit hundreds of villagers in communities living near the mine in Shinyanga region.

Over the years, ABG's mines in Tanzania have invested billions of shillings in education, water, health and infrastructure projects aimed at improving the lives of communities living around its mines.

As part of wide-ranging corporate social responsibility programmes, Bulyanhulu gold mine (BGML) recently donated more than 86.4 million/- to Kakola village for the construction of a dispensary and three classrooms, BMGL said in a statement yesterday.

Kakola, the nearest village in Kahama district to the country's biggest underground gold mine, has enjoyed excellent relations with the Bulyanhulu Gold Mine over the years.

Speaking after the signing of a Memorandum of Understanding with the village, BMGL's acting community relations manager, Theophilo Tweve, said the mine would donate 42,707,750/- for the construction of a dispensary and another 43,702,350/- for the construction of three classrooms.

The Kakola Village Chairman, Emmanuel Bombeda, thanked BGML for its continuous support to the community and promised to utilize the money given for the aimed purpose so that the villagers may benefit from the contribution from the mine towards the improvement of their day-to-day lives.

He also praised previous donations made by the mine to the village, such as investments made in water projects to alleviate chronic water woes at the area.

In a similar development, the BGML General Manager, Dennis Hoof, and other officials from the mine on November 3 this year visited a Muslim school under construction near mine, which has been facilitated by donations from BGML’s Muslim and non-Muslim employees through monthly payroll deductions.

The deductions are voluntary for any BGML employees who wish to donate to the cause.

So far, the school construction project has cost a total amount of 62,757,000/-, with two classrooms already built.

One of the classrooms caters for pre-primary school education with a sitting capacity of 25 Kids, while the other classroom accomodates Standard One pupils with a capacity of 45 children.

Speaking during the visit to the school, the BGML General Manager Dennis Hoof congratulated the Muslim school’s pioneers for establishing such a valued project that will brighten the prospects of future generations.

He advised them to cooperate with the BGML Community Relations Department to discuss the Risk Assessment of the project so as to know exactly where they are, where they want to be, how they are going to reach there and what the risks are.

“If you don’t do risk assessment, the risk of failure is higher and the chance of succeeding is lower,” he stressed.

He promised the mine's continued support to the school after an analysis that will show what the priorities are so as to get the school up and running by early January as planned.

One of the shool's developers, Khalfan Kaboza, who is also a BGML employee, thanked the mine's management for visiting the project and for its continuous support to the development of the community.

African Barrick Gold in September announced that it was tripling its community development spending in Tanzania with the launch of the Maendeleo Fund, which will receive an annual contribution of $10 million to fund projects that improve the quality of life in communities where ABG operates.

It will be the largest corporate community development fund in Tanzania, where about 36 per cent of the population lives below the national poverty line.

ZOEZI LA UGAWAJI WA CHANJO KWA WATOTO LAENDELEA WILAYANI NKASI.

0 comments
Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Joyce Mgana akimuweka alama mtoto Rajabu Wangoma, mwenye umri wa miaka mitatu na miezi minne mara baada ya kupata matone ya Vitamini A, wakati wa uzinduzi wa zoezi la Chanjo ya Surua, Polio, Minyoo na Vitamini A, uliofanyika katika kitongoji cha Mazwi mjini Sumbawanga.

Saturday, November 12, 2011

MBUNGE MO AWEKEZA ZAIDI YA NUSU BILIONI KATIKA MIRADI YA JIMBONI KWAKE MWAKA HUU.

0 comments
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) akizindua mojawapo ya kisima cha maji katika kijiji cha Kibata Kata ya Mtamaa A, kisima hicho kimechimbwa kwa thamani ya zadia ya shilingi milioni 21.
MO akipampu maji katika kijiji cha Kibata tayari kwa matumizi.
Mbunge MO akimtwisha maji mama mmoja mkazi wa kijiji hicho Mariam Juma mara baada ya kuzindua kisima hicho wakati wa ziara yake jimboni humo.
MO akiangalia ujenzi wa msikiti katika Kata ya Utemini ambao unatarajiwa kuwa wa ghorofa moja, katika kuunga mkoni juhudi za waum,ini hao amechangia kiasi cha shilingi milioni 10.
MO akiwagawia nguo baadhi ya watoto wasiokuwa na uwezo wa kijiji cha Itisi mara baada ya kufanya kazi ya akuzindua mradi wa maji safi na salama.
Mbunge MO akizungumza na waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa miradi ya maji katika vijiji 17 ambavyo vimeanza kuchimbwa mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 awamu ya pili, miradi hiyo imemgharimu zaidi ya nusu bilioni.
 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |