Wednesday, September 14, 2011

WATANZANIA WATAKIWA KUNUNUA BIDHAA ZENYE NEMBO YA TABAKA LA OZONI.


Watanzania wametakiwa kununua bidhaa zenye nembo ya tabaka la hewa ya Ozoni (Ozone rafiki) ili kuungana na mataifa mbalimbali duniani kuhifadhi tabaka la hewa hiyo ambalo liko hatarini kutoweka angani kutokana na uchafuzi wa mazingira unaoendelea sasa duniani kote.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yatakayofanyika kitaifa mwezi huu Mjini Arusha, kaimu mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Stephen Nkondakaya amesema kuwa licha ya Tanzania kukabiliwa na changamoto mbalimbali inaendeleza jitihada mbalimbali za kupunguza ongezeko la matumizi ya vifaa vinavyo haribu tabaka la Ozoni angani.

Amesema hali iliyoanza kujitokeza ya kuruhusu kiasi kikubwa cha mionzi ya kikiukaurujuani kufika kwenye uso wa dunia inasabishwa na matumizi ya kemikali hatari zikiwemo “Chlorofluorocarbons”,Halons na Carbon tetrachlorides zinazotumika katika sehemu mbalimbali zikiwemo kwenye majokofu, viyoyozi , vifaa vya kuzimia moto, shughuli za usafishaji vyuma aina zote, utengenezaji wa magodoro, kilimo cha tumbaku na maua zimekuwa chanzo cha uharibifu wa tabaka la Ozoni.

Bw. Nkondokaya amefafanua kuwa hali ya kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi , uharibifu wa macho unaosababisha upofu, upungufu wa kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi kuathirika kwa maumbile na michakato ya ukuaji kunasababishwa na ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabia nchi.

Ameeleza kuwa Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 198 zilizoridhia mkataba wa kimataifa wa Vienna na Itifaki ya Montreal mwaka 1993 inaendelea kuweka mfumo wa udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ikiwemo kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku na vifaa vinavyotumia gesi hizo kama vile majokofu na viyoyozi vilivyokwisha tumika na vinavyotumia vipoozi aina ya R 11 na R 12,kuepuka kutupa ovyo majokofu ya zamani na vifaa vya kuzimia moto vinavyoharibu tabaka la Ozoni aina ya CFCs na halon.

Kuhusu maadhimisho ya Kimataifa ya Tabaka la Ozoni ambayo kitaifa yatakayofanyika Mjini Arusha amesema yataongozwa na kauli mbiu ya “Uondoshaji wa Matumizi ya gesi za “Hydrochrolofluorocarbons”: Mchango muhimu katika kulinda Tabaka la Ozoni na kuzuia Mabadiliko ya Tabianchi” na kuambatana na zoezi la utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulinda tabaka la Ozoni pamoja na kugawa mitambo ya kutambua gesi zinazoharibu tabaka la hewa ya Ozoni kwa wadau wa usimamizi wa sheria ya mazingira nchini.
Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Labels

 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |