Monday, November 14, 2011

Lobby For Special Diaspora Seat, Kalonzo Urges Kenyans Abroad

0 comments
The Kenyan Diaspora should be represented in parliament as recognition of their contribution towards the country’s economy, Vice President, Kalonzo Musyoka has proposed.

Addressing Kenyans in East London in the UK on Sunday night, Mr Musyoka urged Kenyans wherever they are in the Diaspora to lobby their MPs in changing the law so that a provision of a special Diaspora seat could be created to accommodate those living away from home into local leadership and politics.

"The Diaspora remits a huge amount of money to Kenya’s economy every year and your participation in national building in this particular way should be recognised," the Vice-President said amidst thunderous applause.

He said that the foreign exchange remittance by the Diaspora increased by 27 per cent from $350.9million to $475million. In the month of October alone, Kenyans living abroad remitted Ksh 8.8billion, which was more than an annual budget for most government ministries.

He said that the duo-citizenship provision in the new constitution should assure Kenyans that they still have a role to play in the development of Kenya.

He said that he was ready to work with the Diaspora in ensuring that their interests in Kenya were recognised.

He was accompanied by the Minister for Special Programmes, Esther Murugi, Assistant Ministers, Kabando wa Kabando, Ephraim Maina, Asman Kamama, and the Government Chief Whip, Johnstone Muthama as well as the Permanent Secretary in the office of the Home Affairs, Dr Ludeki Chweya.

Mr Maina said that he supported either the presidency of Musyoka, George Saitoti or Uhuru Kenyatta, saying they were the most experienced.

Mr Kabando said that it would be wrong for some elderly politicians from Central province to purport that they speak for the whole community especially on the issue of whom to support in the next presidential elections.

Musyoka’s meeting with Kenyans abroad comes at a time when the Prime Minister Raila Odinga’s supporters announced a major campaign network in Kenya, America and Europe aimed at targeting the 3.4 million potential voters from the Diaspora.
Source: The Standard

Dreamliner to Make Debut Landing at JKIA

0 comments
The Dreamliner Boeing 787 — which first took to the skies in September — will make its debut landing at the Jomo Kenyatta International Airport before the end of the year.

A team from Kenya Airways is expected to fly in the plane, which would carry selected passengers for a short flight to give travellers a taste of the Dreamliner experience.

Kenya Airways has an order for nine Dreamliners, with the option to take four. The first of its order is expected in October 2013, two years behind schedule.

The company is looking to increase its fleet to more than 100, move to new destinations and increase frequencies on lucrative routes over the next 10-years.

To achieve this growth strategy, the airline expects to raise part of the money in a rights issue. The date and amount of money the airline wants to raise are yet to be made public.

However, a note from NIC Securities, said KQ is expected to raise at least Sh23 billion. It predicts that the airline may discount its share by up to 22 per cent in the rights issue. This would put the price at about Sh20 a share.

Alex Mbugua, KQ’s financial director, told investors last month that part of the money raised would go towards pre-delivery payments for the Dreamliner. Airlines are expected to make payments for aircraft two years before delivery.

“The first pre-delivery payment should have gone last month and that is why we are coming to the market now,” he said.
Source: Business Daily Africa

Tanzania State Organs On Alert Over Nuclear Threat

0 comments
Dar es Salaam — Police and other state organs are on the alert against illegal trafficking of nuclear materials into the country, the Director of Criminal Investigations (CID), Mr Robert Manumba has confirmed.

He said several incidents where such radioactive materials have been brought into Tanzania or those legally acquired fell into the wrong hands, but much concern would come when uranium mining starts shortly in various deposits found in the country.

"Some people have been caught in illegal possession of nuclear materials. Our scientific experts must work closely with the police to ensure the situation is brought to control," he told reporters after closing a week-long training course on combating illicit trafficking in radioactive materials for police officers from various African states.

He said police are worried with the mining of uranium, a radioactive mineral, set to commence in due course, there was a likelihood of nuclear materials, which are hazardous to people's health, falling into wrong hands of illegal traffickers or improperly trained practitioners.

He emphasised that police need specialised training on how to handle nuclear materials and deal with those involved in illegal trafficking. He added that a random survey have found out that some traffickers were transporting radioactive materials in ordinary bags, exposing people to the dangers.

The CID chief specifically called on experts working with the Tanzania Atomic Energy Commission (Taec) to work closely with the police who are not yet well versed with the dangers posed by nuclear hazards or uranium and other radioactive minerals soon to be mined in the country.

Speaking when closing the training attended by over 40 senior police and intelligence officers from 22 African countries, Mr Manumba cited unlawful possession, use, transfer, alteration and dispersal of radioactive materials as potential sources of danger that can cause death and injuries to people.

"They may also include theft or robbery or radioactive materials. They may also include embezzlement or fraudulent obtaining of the materials. All these acts are criminal which can be minimised or eliminated by an effective legal enforcement," he pointed out.

However, he noted that eventual success in prosecution of the suspects would always depend on how the frontline officers (police and experts in nuclear technology) were legally competent in preparing investigations and prosecutions.

A nuclear security expert from the Vienna-based International Atomic Energy Agency (IAEA) Adam Bacheller, said the course was among a series of activities taken by the specialised UN body to create awareness among the law enforcement agencies in Africa on the nuclear hazards.

"Illegal trafficking of radioactive materials, radiation control and proper handling of nuclear materials are key areas of concern for many countries, especially known for terrorism threats across the globe," he said.
Taec acting director general Firmin Banzi, said the police and intelligence officers have been acquainted with new skills and experiences which was important tools in fighting the growing global threat of illicit trafficking of radioactive materials.

Recently, Taec warned against lack of effective protection measures in the industries, mines and other work places where radiation technology is used and closed 30 X-ray centres for failure to abide by the safety measures.

It says lack of effective radiation protection infrastructures posed occupational risks to workers through exposure to ionising radiation. The state-run agency said although Tanzania has seen increased use of nuclear techniques such as the atomic energy, many facilities possessed and used throughout the country lacked effective radiation control.
Source The Citizen.

Govt to Spend $165 Million On Agriculture

0 comments
The Tanzania Government is set to use more than 165.6 million in seven years to implement the Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance Support rogramme (MIVRFS).

The program will benefit more than 15 million people in the country which will be implemented by Tanzania in collaboration with the International Fund for Agricultural Development (IFAD), Africa Development Bank (ADB), and Alliance for Green Revolution in Africa (AGRA).

"The program will be implemented in a period of seven years from 2011-2018 where it also aims at empowering small and mid-sized entrepreneur rise their capital," said William Lukuvi, the Minister of State for Policy in the Prime Minister's Office.

The programme will be directed to benefit over 250,000 farmers and 16,500 groups of small scale entrepreneurs.

He said the (MIVRFS) programme will be an instrument of structuring markets, giving value to agriculture products and create awareness to agriculturalists, and monitoring of rural funds through Governmental and Non- governmental organizations spread across the country.

The program also aims at increasing financial services to the people by improving NGO's and community banks.

It will handle provision of loans to the agricultural sector with the help of commercial banks to the tune of $218.7million, the Minister explained.
Ms.Tonia Kandiero, the Resident Representative of African Development Bank in Tanzania told The East African Business Week in Dar es Salaam that the programme comprises three major components namely: Marketing Infrastructure and Systems Development; Rural Finance and Programme Coordination; plus Management to be financed by the three stakeholders of ADF, IFAD and AGRA.

She said that out of $165.6 million, AfDB will provide about $62 million to the programme, while IFAD will contribute about $91.0 million, and AGRA will inject some $7.3 million. According to the AfDB, the Marketing Infrastructure and Value Addition activities of the programme will be implemented in 32 districts (out of 129) in 16 regions.

ZIARA YA RAIS DK SHEIN SHARJAH (UAE) .

0 comments
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kumbusho la Dr.Sultan Al –Qasimi, Mjini Sharjah,(kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa kumbusho Ali Almarri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi,Prof.Hassam Hamdy,(kushoto) alipotembelea Chuoni hapo Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi,Prof.Hassam Hamdy,(kushoto) na (kulia) Sheikh Salim Bin Abdulrahman Al Qasimi,Meneja Mkuu wa Ofisi ya Mfalme,alipotembelea katika chumba mafunzo ya udakatari Chuoni hapo Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mhe Sheikh Sultan Mohamed Al Qasimi,alipowasili katika makaazi yake Mjini Sharja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiongozana na Makamo Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi,Prof.Hassam Hamdy,(kulia) na (wa pili kushoto) Sheikh Salim Bin Abdulrahman Al Qasimi,Meneja Mkuu wa Ofisi ya Mfalme, alipotembela chuo cha Afya ya sayansi ya Sayansi Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi,Prof.Hassam Hamdy,(wa pili kulia) na (kushoto) Sheikh Salim Bin Abdulrahman Al Qasimi,Meneja Mkuu wa Ofisi ya Mfalme,alipotembelea katika chumba mafunzo ya udakatari Chuoni hapo Mjini Sharjah,(wa kwanza kushoto) Waziri wa Kazi,uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika Mhe Haroun Ali Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi,Prof.Hassam Hamdy,(kushoto) na (kulia) Sheikh Salim Bin Abdulrahman Al Qasimi,Meneja Mkuu wa Ofisi ya Mfalme,alipotembelea katika chumba mafunzo ya udakatari Chuoni hapo Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kumbusho Ali Almarri,wakati alipotembelea kumbusho la Dr.Sultan Al –Qasimi, Mjini Sharjah,Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo alipotembelea kuona mambo ya kihistoria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kumbusho Ali Almarri,wakati alipotembelea kumbusho la Dr.Sultan Al –Qasimi, Mjini Sharjah,Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo alipotembelea kuona mambo ya kihistoria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa wa wakumbusho Ali Almarri,wakati alipotembelea kumbusho la Dr.Sultan Al –Qasimi, Mjini Sharjah,Mjini Sharjah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia baadhi ya vifaa , alipotembelea kuona mambo ya kihistoria wakati alipotembelea kumbusho la Dr.Sultan Al –Qasimi, Mjini Sharjah,Mjini Sharjah,(kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa kumbusho Ali Almarri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mhe Sheikh Sultan Mohamed Al Qasimi,alipowasili katika makaazi yake Mjini Sharja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda wa Ras Al Khaimah,Mjini Sharjah,(kulia) ni Mwenyekiti Ahmed Mohammed Al Midfa, na (kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Mhe Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akuipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanya bishara,wenyeviwanda Amed Mohammed Al Midf,alipotembelea kituo cha jumuiya hiyo na kuangalia baadhi ya bidhaa mbali mbali katika kituo hicho,Mjini Sharjah.Picha na Ramadhan Othman,Sharjah (UAE)

WAFANYAKAZI EXIM WAJUMUIKA KTK BONANZA LA FAMILIA

0 comments
Meneja Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Dinesh Arora akishiriki
mchezo wa kubeba mdomoni yai katika kijiko bila kuliangusha katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo loililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakishiriki katika
mchezo wa kutembea ndani ya gunia katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakishiriki katika
mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu


BENKI ya Exim Tanzania imefanya bonanza la siku ya familia kwa wafanyakazi wake katika kuwapongeza na kuongeza ari ya kazi itakayoimarisha utendaji wa benki hiyo. Wafanyakazi wa matawi mbalimbali yaliyopo Dar es Salaamjuzi walijumuika pamoja katika ufukwe wa Wet and Wild Beach, Kunduchi Dar es Salaam ambapo pamoja na mingine michezo ya kuvuta kamba, mpira wa pete, miguu, kufukuza kuku na kucheza dansi vilichukua nafasi kubwa ya bonanzahilo.


Akizungumza Meneja Mkuu wa benki hiyo Ginesh Arora alisema kuwa bonanza hilo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano pamoja na kujenga upendo wa kikazi baina ya wafanyakazi.


Alisema kuwa benki hiyo kuwa katika benki mojawapo zinazokuwa kwa kasi nchini ni matokeo mazuri yanatokana na nguvu ya pamoja ya wafanyakazi katika matawi yao nchi nzima hivyo wakati fulani ni lazima nguvu hiyo ikutanishwe pamoja katika kufahamiana na kuimarisha umoja walionao.


Arora alisema ni utaratibu ambao benki imejiwekea kuwakutanisha wafanyakazi wake mara tatu kila mwaka ikiwa ni katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata nafasi kufurahia mafanikio pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi ndani ya benki.
"Ni bonanza la kufahamiana na kudumisha umoja na urafiki wa kikazi baina ya wafanyakazi, leo hapa wote ni wamoja bila kujali vyeo vyetu makazini, tunacheza, kunywa na kuogelea", alisema Arora.


Kwa upande wake Baraka Enock wa tawi la Namanga kitengo cha operesheni ambaye alishiriki katika mchezo wa mpira wa wavu alisema bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kudumisha ushirikiano wa kikazi miongoni mwao. Alisema kutokana na majukumu mengi ya kikazi wakati fulani unaweza usimfahamu mfanyakazi mnayefanya tawi moja hivyo bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kuburudika na kudumisha mahusiano.


Katika baadhi ya michezo iliyochezwa, timu ya soka ya Exim Makao Makuu iliingia fainali na kuichapa bila huruma Exim Matawi kwa bao 1-0 mchezo ambao ulijaa ushindani mkubwa pamoja ushabiki.

SALAMA JABIR AJA UPYA,AIBUKA NA MKASI TV SHOW

0 comments
MTANGAZAJI MAARUFU SALAMA JABIR ANARUDI KIVINGINE NA KIPINDI KIPYA KABISA KINACHOITWA MKASI KITAKACHOKUWA KIKIRUSHWA HEWANI KILA SIKU YA JUMATATU KUANZIA SAA 3:30 USIKU. KIPINDI HICHI KITAANZA KUONEKANA HEWANI KUPITIA EAST AFRICA TV KUANZIA TAREHE 14 MWEZI NOVEMBA 2011.


KIPINDI HICHO KITAKUWA KIKIFANYIKIA SALOON NA KUHOJI WATU MBALI MBALI WENYE VIPAJI LUKUKI KUHUSIANA NA MAISHA YAO BINAFSI NA HII NI KWA MARA YA KWANZA KUFANYIKA KATIKA HISTORIA YA VIPINDI VYA AFRIKA YA MASHARIKI KUTOKANA NA MTIRIRIKO MZIMA WA KIPINDI ULIVYO NA MANDHARI YAKE.


USIKOSE KUTAZAMA LUNINGA YAKO ILI KUPATA KILICHO BORA KUTOKA KWA SALAMA JABIR.
NI ‘MKASI’ UTAKAOTIKISA TANZANIA NA AFRIKA YA MASHARIKI KWA UJUMLA.
KUMBUKA NI KILA JUMAATATU SAA TATU NA NUSU USIKU

ZIARA YA MO KATIKA MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA UNAOFADHILIWA NA BADEA SINGIDA MJINI.

0 comments
Mo Dewji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa mradi huo wa BADEA ambao unatarajiwa kumalizika Julai mwakani.
Mo Dewji akipata maelezo ya sehemu mbalimbali ndani ya eneo la Ujenzi la mradi wa Tanki kubwa na la kisasa kutoka kwa mmoja wa wataalum wa kampuni ya Spencon Service Ltd alipotembelea huko eneo la Mandewa.
Mkurugenzi wa SUWASA,Injinia Isaack Nyalonji Akitoa maelezo ya kisima kikubwa cha mradi wa BADEA katika eneo la Mwankoko, kushoto kwake Mbunge Mo Dewji alipotembelea kukagua mradi huo ambao unatarajia kumalizika Julai mwakani. Wa pili kushoto, Mstahiki Meya, Shehe Salum Mahami, eneo la chanzo cha mradi huo wa maji.



Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji amesema ataendelea kuhakisha anapigania kumaliza tatizo la maji kwenye jimbo hilo ikiwemo kupambana nalo mpaka ngazi ya juu wakiwemo wanaokwamisha mradi huo.

Dewji alisema hayo mapema leo wakati alipotembelea mradi wa uboreshaji wa huduma za Maji Safi na Salama Singida Mjini unaofadhiliwa na Benki yaMaendeleo ya Kiarabu (BADEA), Serikali na mashirika mengine yakiwemo Shirika la Mafuta ulimwenguni (OFID) unaogharimu dola za kimarekani bilioni 17.2(SHILINGI 25,800,000,000,00) mpaka kukamilika kwa mradi huo.

Alisema kua,mradi huo ambao ulianza kuombwa tokea miaka 10 iliyopita na kuja kukubaliwa mwaka 2009, umekumbwa na changamoto mbalimbali hali iliyopelekea kushindwa kukamilika kwa wakati hivyo kuahidi kuonana na viongozi wa juu akiwemo Waziri mwenye dhamana na Rais ilikuondoa tatizo lililokuwepo.

“Nimepokea taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) na kudai kuwa miongoni mwa changamoto hizo kwa mradi huo ni kupita kwenye sehemu za hifadhi ya barabara na katika makazi ya watu, suala hili nitalishughulikia kuona tunafika wapi ikiwemo kuonana na waziri mwenye dhamana” alisema Dewji.

Kwa upande wake Injiania Isaack Nyakonji wa SUWASA alisema mbali na matatizo ya mradi huo kupita kwenye hifadhi ya barabara na makazi ya watu, pia hali ya ukame na tatizo la umeme limechangia kusuaua kwa mradi huo.
“Singida ndani ya miaka miwili tulikuwa na ukame sambamba na ukatikaji wa umeme hali hiyo ilipelekea mradi huu kusimama. Pia mabadiliko ya gharama ya mradi huu yameongezeka kutokana na mazingira kuwa magumu” alisema Eng.Nyakonji.

Katika ziara hiyo, Dewji alitembelea sehemu mbalimbali ya mradi huo maarufu kama BADEA na kujionea utendaji wa kazi ikiwemo eneo la visima Mwankoko na sehemu ya tanki kubwa na la kisasa ambalo likikamilika litasaidia kupunguza shida ya maji Singida Mjini.

MH. MO AMPONGEZA MKWASA NA KUISIFU TFF KWA KUONYESHA UZALENDO

0 comments

AMTAKA MKWASA KUWAPA RAHA WATANZANIA.

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MJINI MH. MOHAMMED DEWJI AMETOA PONGEZI ZA DHATI KWA KOCHA WA SIKU NYINGI HAPA NCHINI CHARLES BONIFACE MKWASA KWA KUCHAGULIWA KUWA KOCHA MKUU WA TIMU YA SOKA YA TAIFA ‘TAIFA STARS’.

MH.MBUNGE HUYO ALMAARUFU KAMA ‘ MO’ AMBAYE ANASIFIKA KWA KUHAMASISHA MICHEZO PIA AMELISIFU SHIRIKISHIO LA MPIRA WA SOKA TANZANIA (TFF) KWA KUONYESHA UZALENDO KWA KUMCHAGUA KOCHA WA HAPA NYUMBANI KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA.

PONGEZI HIZO AMEZITOA KUFUATIA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA TFF BW. ANGETILE HOSIAH ALIYOITOA SIKU YA JUMAMOSI KWA VYOMBO VYA HABARI KUWA MKWASA ALIYEKUWA AKIIFUNDISHA TIMU YA TAIFA YA SOKA YA WANAWAKE YA TANZANIA ‘TWIGA STARS’ AMECHAGULIWA KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA BARA.

KATIKA UTEUZI HUO KOCHA MACHACHARI ANAYEFUNDISHA TIMU YA COASTAL UNION YA TANGA JAMHURI KIHWELO ‘JULIO’ AMETEULIWA KUWA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA SIMBA KHALID ABEID AMECHAKUGULIWA KUWA MENEJA MPYA WA TIMU HIYO WAKATI WA MICHUANO YA CECAFA ITAKAYOFANYIKA KATIKA MIJI YA DAR ES SALAAM NA MWANZA KUANZIA NOVEMBA 25 HADI DISEMBA 10 MWAKA HUU.

KATIKA PONGEZI HIZO MH. ‘MO’ AMESEMA KWA HAKIKA TFF IMEONYESHA UZALENDO NA KUMTAKIA MKWASA MAFANIKIO PINDI ATAKAPOANZA JUKUMU LA KUONGOZA JAHAZI LA TIMU YA TAIFA.

AIDHA MH. ‘MO’ AMEITAKIA MAFANIKIO MEMA TIMU YA TAIFA IKIWA CHINI YA KOCHA MKWASA HUKU AKISEMA ‘ MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TAIFA STARS, MUNGU MBARIKI MKWASA NA KAMATI NZIMA YA UFUNDI YA TIMU HIYO.

MVUA YASABABISHA BALAA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JIJINI MWANZA

0 comments
Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne bila kupumzika imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga kutokana na maji mengi kujaa katika uwanja wa ndege wa jijini humo.kama ionekanavyo pichani hapa.
Ngazi Maalum zinazotumika kapandia abiria kwenye ndege kama zinavyoonekana kutokana na mafuriko yaliyoikumba airport ya jijini Mwanza leo mara baara ya mvua kubwa kunyesha.
Hakuna Ndege yeyote iliyoondoka wala kutua leo jijini Mwanza maana hali ilikuwa ni mbaya sana.
Hapa leo hakukuwa na kazi yoyote nyingine leo.
Sehemu ya kurukia Ndege ikiwa imeharibika vibaya kutokana na Maji ya Mvua iliyonyesha siku ya leo Jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakiendelea kufanya taratibu ya kuweka vitu sawa katika chumba cha kupita abiria wanaosafiri.huku maji yakiwa yameingia mpaka ndani.
Ndege zilizofanikiwa kuruka katika uwanja huo wa Mwanza ni hizi tu,lakini zile za abiria hakuna hata moja iliyoweza kuondoka wala kutua.
Wafanyakazi mbalimbali wa kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda katika eneo hilo.
Ilikuwa ni kama bahari ndogo katika kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza leo.

BUNGENI DODOMA LEO

0 comments
Wabunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati (kushoto) na Lediana Mng'ong'o wakiteta kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole- Sendeka kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.

.

JUMLA YA SH. BILIONI 1 NA MILLIONI 100 ZIMEKUSANYWA NA KAMATI YA TAIFA YA MAAFA ZANZIBAR KUFUATIA AJALI YA MELI YA MV. SPICE ISLANDER

0 comments
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar
Mh. Mohammed Aboud Mohammed
NA IDARA YA HABARI MAELEZO - ZANZIBAR

Jumla ya Sh. Bilioni 1 na Millioni 100 zimekusanywa na Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar hadi kufikia leo ikiwa ni michango mbalimbali kutoka kwa Taasisi, Watu binafsi na Wadau mbalimbali wa nje na ndani ya Zanzibar kutokana na ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati alipokuwa akipokea Mchango wa Dola za Kimarekani 1,444 sawa na Sh. Milioni 2 laki Moja na Hamsini na Nne na Mia Nane kutoka kwa Watafiti mbalimbali kutoka nje.

Waziri Aboud amesema kuwa Serikali imefarijika sana kutokana na wanafunzi hao kuona umuhimu wa kutoa michango hiyo kwa waathirika wa ajali hiyo ya Meli ya Mv. Spice Islanders.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi sasa bado haijatumia fedha yoyote ile iliyotolewa kwa Michango hiyo ambapo fedha hizo zinatarajiwa kutolewa mara tu Tume ya Uchunguzi ya Ajali hiyo iliyoteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutoa taarifa yake.

Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya Watafiti hao Dk. Naiman Saleh Jidawi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Baharini Zanzibar kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa wanafunzi hao wameguswa sana na ajali hiyo hivyo wameona na wao watoe mchango wao.

Aidha amesema kuwa Fedha hizo walizochangia zitasaidi katika malengo yaliyokusudiwa kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuwa watafiti hao kutoka nje walishtushwa sana na tukio la ajali ya Mv. Spice Islandes hivyo ikawalazimu kujikusanya pamoja na kuona kuwa wao hawatajisikia vizuri ikiwa hawatochangia chochote kuhusiana na ajali hiyo ambayo siyo ya Zanzibar tu bali ni ya Tanzania kwa ujumla.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZINDUA KAMPENI YA CHANJO KWA WATOTO WILAYANI NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

0 comments
Mratibu wa Kinga ya Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Peres Kamugisha (kulia) akipokea mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa mwaka huu,Elisha Lawrence Gama,mara baada ya kuwasili wilayani humo hivi karibuni.
Mkimbiza Mwenge kitaifa mwana huu,Elisha Lawrence Gama akitoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika viwanja vya CCM wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akijiandaa kumpa tone la vitamini A mtoto wa miaka 2 Athumani Idd baada ya kuzindua zoezi la chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wilayani Namtumbo hivi karibuni.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akimpatia tone la vitamini A mtoto Suzy Lucas Njela ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa zoezi la chanjo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hivi karibuni,ambapo Wilaya hiyo imekusudia kutoa chanjo ya magonjwa mbalimbali kwa watoto zaidi ya 143,133 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na wilaya zingine za mkoa huo.Picha na Muhidini Amri - Ruvuma.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATEMBELEA MAONYESHO YA MIAKA 50 YA UHURU KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE SONGEA.

0 comments
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kulia) akisisitiza jambo wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye ufunguzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru ambazo kimkoa zilifanyika katika viwanja vya nane nane mjini songea.Kushoto ni Dkt. Ngowi wa hospitali ya mkoa songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Said Mwambungu akiangalia moja ya viatu vilivyotengenezwa kwa kutumia ngozi ya mbuzi na mafundi kutoka muungano wa viwanda vidogo nchini (MUVI) zamani sido mkoani humo wakati wa maonyesho ya ufunguzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika katika viwanja vya nane nane mjini songea.kulia ni Kaimu Meneja wa ISDO mkoa wa Ruvuma,Richard Mbambe.Picha na Muhidin Amri-Ruvuma.

KIKAO CHA MAKAMISHNA WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA CHAANZA DAR HII LEO.

0 comments
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,Jaji Prof. Ibrahim Juma (wa kwanza kushoto) akiongoza kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume jijini Dar es Salaam leo.
Makamishna wa Tume hiyo wakiwa katika kikao leo.

ZIARA YA BALOZI SEIF ALI IDDI MKOANI SINGIDA

0 comments
MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM,BALOZI SEIF ALI IDDI AKIWA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SINGIDA ND. JORAM ALUTE NA MBUNGE WA VITI MAALUM CCM MH. DIANA KILOLO MARA BAADA YA MAPOKEZI YA BALOZI SEIF KUFUATIA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA MKOANI SINGIDA.
WASANII WA IGUGUNO WILAYANI IRAMBA MKOA WA SINGIDA WAKIMLAKI MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM,BALOZI SEIF AMBAYE ALIKUWEMO WILAYANI HUMO KUWAAGA BAADA YA KUMALIZA UTUMISHI WAKE WA KUWA MLEZI WA MKOA HUO KICHAMA.
MJUMBE WA KAMATI YA SIASA YA MKOA KASKAZINI UNGUJA AMBAYE PIA NI MKE WA BALOZI SEIF MAMA ASHA SULEIMAN IDDI AKISALIMIANA NA WANA CCM WA ILONGELO SINGIDA VIJIJINI.KATIKA MKUTANO HUO MAMA ASHA ALIAHIDI KUTOA SETI MOJA YA JEZI NA MIPIRA KWA TIMU YA VIJANA WA ILONGELO ILI KUENDELEZA MICHEZO. KULIA KWAKE NI KATIBU WA CCM SINGIDA VIJIJINI ND. JOSEPH RUDISHA NA KUSHOTO KWAKE NI KATIBU WA CCM MKOA SINGIDA MAMA NAOMI JEREMIA KAPAMBALA.

Tanzania itaendelea kuwa ya amani na usalama kufuatia Wananchi wake waliowengi kupenda tabia hiyo licha na baadhi ya watu wachache kujaribu kuvuruga sifa hiyo ambayo imejijengea Ulimwenguni.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akiwa katika ziara ya Kuwaaga wana CCM wa Mkoa wa Singida kwenye Mikutano mbali mbali ya Kiwilaya baada ya kumaliza Utumishi wa Kuwa Mlezi wa Mkoa huo Kichama.

Balozi Seif alisema Mshikamano wa Watanzania unaoendelea kuonyeshwa huku wakizingatia umuhimu wa amani umeleta faraja ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kuwaomba wananchi kutokubali kuhadaiwa katika kuichezea Amani.

Alisema jamii inapaswa kuyaepuka makundi na baadhi ya watu wanaoshawishi Wananchi na hawa Wanafunzi wa elimu ya Juu kupinga au kufanya Maandamano dhidi ya Serikali kwa lengo la kuvuruga amani ya Nchi.

Aliahidi kwamba CCM bado inapendwa na itaendelea kuwa na nguvu kutokanana na Sera zake, hivyo bila ya Chama hicho amani haitaendelea kuwepo.

“ Mtu wa fujo ataendeleaje kuongoza Nchi bila ya fujo ”. Alihoji Balozi Seif Ali Iddi.

Amewaasa wana CCM kuwepuka Makundi ndani ya Chama ambayo wakati mwingi husababishwa na Fedha zinazotolewa na Baadhi ya Wanachama wakati wanapoomba Uongozi.

Aliomba kuondoshwa kwa makundi ndani ya chama kwa vile ndio yanayoleta mashimo.

Akizungumzia suala la Mchakato wa Katiba ya Jamukuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Seif aliwaomba Wananchi kutoa Maoni yao wakati utakapowadia wakizingatia zaidi Msimamo utakaotolewa na Chama chao.

Alisema Bunge linaanza kujadili Rasimu ya muswaada wa sheria utakaomuewezesha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Tume itakayopokea Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka.

“ Mnapaswa kuwa na hadhari na makini na baadhi ya watu wanaoanza kujadili Muundo wa Katiba Mpya wakati hata hiyo tume haijaundwa. Huko ni kupotosha Wananchi ”. Alisisitiza Balozi Seif.

Balozi Seif Ali Iddi ambaye amefanya ziara ya kuaga katika Wilaya za Iguguno, Ilongero na Singida Mjini ndani ya Mkoa wa Singida anatarajiwa kuripoti rasmi kuwa mlezi Mpya wa CCM Mkoa Mjini Magharibi mnamo tarehe 19/11/2011.

MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI AFUNGUA MAFUNZO YA WAKAGUZI WA NDANI LEO JIJINI DAR

0 comments
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mohamed Mtonga akifungua mafunzo ya wakaguzi wa ndani leo jijini Dar es salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi ili waweze kuendana na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania.
Wakaguzi wa Ndani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mohamed Mtonga mara baada ya kufungua mafunzo ya wakaguzi wa ndani leo jijini Dar es salaam yenye lengo kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi ili waweze kuendana na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania.Picha na Tiganya Vincent Dar es salaam.

Maelezo Na Glady Sigera-Dar es salaam.

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Internal Auditor General imeendesha mafunzo ya siku moja kwa wakaguzi wa Ndani ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ubora unaokubalika kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa na kuleta tija.

Akifungua mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga alisema kuwa mafunzo hayo yatawashirikisha wakaguzi wote wa serikali na wale wa Serikali za mitaa Halmashauri hapa nchini.

Alisemakuwa mafunzo hayo yanalenga kuwapa mwanga wakaguzi wa ndani pamoja na kuwaelezea umuhimu wa vitabu vya mwongozo wa ukaguzi wa ndani ambavyo ni kwa ajili ya ukaguzi wa ndani katika taasisi za umma nchini.

Mtonga aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwawezesha wakaguzi wa ndani kupata mbinu mbalimbali za kisasa za ukaguzi ambazo zinakwenda sanjari na viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndani ambapo Tanzania imeridhia kutumia viwango hivyo kuanzia mwezi Julai 2011.

Alisema kuwa katika mafunzo hayo wakaguzi hao watajifunza mchakato mzima wa ukaguzi ,kuandaa mpango wa ukaguzi na utoaji wa taarifa za ukaguzi.

Maeneo mengine ni utekelezaji wa ukaguzi , uwekaji wa kumbukumbu wa kazi ya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa mchakato mzima wa ukaguzi.

Aidha , Mtonga alisema kuwa wakaguzi hao wanapaswa kuchukua miongozo kama vitendea kazi ambavyo ni endelevu na ni sehemu ya nyaraka muhimu za kufanyia kazi kwa wakaguzi wa ndani wakati wakitekeleza majukumu yao ya ukaguzi wa ndani.

Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania yametoka kukamilika kwa vitabu vya mwongozo wa ukaguzi wa ndani uliondaliwa na wataalam elekezi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao.

Blog Archive

Labels

 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |