Monday, November 14, 2011

MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI AFUNGUA MAFUNZO YA WAKAGUZI WA NDANI LEO JIJINI DAR


Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mohamed Mtonga akifungua mafunzo ya wakaguzi wa ndani leo jijini Dar es salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi ili waweze kuendana na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania.
Wakaguzi wa Ndani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mohamed Mtonga mara baada ya kufungua mafunzo ya wakaguzi wa ndani leo jijini Dar es salaam yenye lengo kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi ili waweze kuendana na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania.Picha na Tiganya Vincent Dar es salaam.

Maelezo Na Glady Sigera-Dar es salaam.

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Internal Auditor General imeendesha mafunzo ya siku moja kwa wakaguzi wa Ndani ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ubora unaokubalika kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa na kuleta tija.

Akifungua mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga alisema kuwa mafunzo hayo yatawashirikisha wakaguzi wote wa serikali na wale wa Serikali za mitaa Halmashauri hapa nchini.

Alisemakuwa mafunzo hayo yanalenga kuwapa mwanga wakaguzi wa ndani pamoja na kuwaelezea umuhimu wa vitabu vya mwongozo wa ukaguzi wa ndani ambavyo ni kwa ajili ya ukaguzi wa ndani katika taasisi za umma nchini.

Mtonga aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwawezesha wakaguzi wa ndani kupata mbinu mbalimbali za kisasa za ukaguzi ambazo zinakwenda sanjari na viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndani ambapo Tanzania imeridhia kutumia viwango hivyo kuanzia mwezi Julai 2011.

Alisema kuwa katika mafunzo hayo wakaguzi hao watajifunza mchakato mzima wa ukaguzi ,kuandaa mpango wa ukaguzi na utoaji wa taarifa za ukaguzi.

Maeneo mengine ni utekelezaji wa ukaguzi , uwekaji wa kumbukumbu wa kazi ya ukaguzi na uhakiki wa ubora wa mchakato mzima wa ukaguzi.

Aidha , Mtonga alisema kuwa wakaguzi hao wanapaswa kuchukua miongozo kama vitendea kazi ambavyo ni endelevu na ni sehemu ya nyaraka muhimu za kufanyia kazi kwa wakaguzi wa ndani wakati wakitekeleza majukumu yao ya ukaguzi wa ndani.

Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Japan na Serikali ya Tanzania yametoka kukamilika kwa vitabu vya mwongozo wa ukaguzi wa ndani uliondaliwa na wataalam elekezi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao.

Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Labels

 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |