Kuzungumzia na uthibitisho wa ujio wa Mwanamuziki huyo Dar,Meneja wa Masoko wa kampuni ya G5 CLICK COMPANY,Desy Ernest amesema kuwa,Mwanamuziki Jaguar kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la BODA KWA BODA BEACH CONCERT litalofanyika kaika fukwe ya Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar Es Salaam LEO majira ya saa moja jioni huku akisindikizwa jukwani na wasanii wakibongo wakiwemo Sumalee,GodZilla,Country Boy & Stamina,Young D,Beka na wengineo wengi tu
Desy Ernest amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za BODA KWA BODA BEACH CONCERT zitakuwa tofauti na zenye msisimko mkubwa, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani ya Tanzania.
Jaguar awasihi mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ilikukamilisha mpango mzima wa BODA KWA BODA BEACH CONCERT.






0 comments:
Post a Comment