Monday, November 14, 2011

WAFANYAKAZI EXIM WAJUMUIKA KTK BONANZA LA FAMILIA


Meneja Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Dinesh Arora akishiriki
mchezo wa kubeba mdomoni yai katika kijiko bila kuliangusha katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo loililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakishiriki katika
mchezo wa kutembea ndani ya gunia katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakishiriki katika
mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la familia la wafanyakazi wa benki hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kunduchi Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu


BENKI ya Exim Tanzania imefanya bonanza la siku ya familia kwa wafanyakazi wake katika kuwapongeza na kuongeza ari ya kazi itakayoimarisha utendaji wa benki hiyo. Wafanyakazi wa matawi mbalimbali yaliyopo Dar es Salaamjuzi walijumuika pamoja katika ufukwe wa Wet and Wild Beach, Kunduchi Dar es Salaam ambapo pamoja na mingine michezo ya kuvuta kamba, mpira wa pete, miguu, kufukuza kuku na kucheza dansi vilichukua nafasi kubwa ya bonanzahilo.


Akizungumza Meneja Mkuu wa benki hiyo Ginesh Arora alisema kuwa bonanza hilo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano pamoja na kujenga upendo wa kikazi baina ya wafanyakazi.


Alisema kuwa benki hiyo kuwa katika benki mojawapo zinazokuwa kwa kasi nchini ni matokeo mazuri yanatokana na nguvu ya pamoja ya wafanyakazi katika matawi yao nchi nzima hivyo wakati fulani ni lazima nguvu hiyo ikutanishwe pamoja katika kufahamiana na kuimarisha umoja walionao.


Arora alisema ni utaratibu ambao benki imejiwekea kuwakutanisha wafanyakazi wake mara tatu kila mwaka ikiwa ni katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata nafasi kufurahia mafanikio pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi ndani ya benki.
"Ni bonanza la kufahamiana na kudumisha umoja na urafiki wa kikazi baina ya wafanyakazi, leo hapa wote ni wamoja bila kujali vyeo vyetu makazini, tunacheza, kunywa na kuogelea", alisema Arora.


Kwa upande wake Baraka Enock wa tawi la Namanga kitengo cha operesheni ambaye alishiriki katika mchezo wa mpira wa wavu alisema bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kudumisha ushirikiano wa kikazi miongoni mwao. Alisema kutokana na majukumu mengi ya kikazi wakati fulani unaweza usimfahamu mfanyakazi mnayefanya tawi moja hivyo bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kuburudika na kudumisha mahusiano.


Katika baadhi ya michezo iliyochezwa, timu ya soka ya Exim Makao Makuu iliingia fainali na kuichapa bila huruma Exim Matawi kwa bao 1-0 mchezo ambao ulijaa ushindani mkubwa pamoja ushabiki.
Kindly Bookmark this Post using your favorite Bookmarking service:
Technorati Digg This Stumble Stumble Facebook Twitter
YOUR ADSENSE CODE GOES HERE

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Labels

 

Pages

Popular Posts

BBC Xclusives

| BongoXclusive © 2009. All Rights Reserved | Sponsored by: Website Templates | Premium Wordpress Themes | consumer products. Thanks to blogger template
Template Style by My Blogger Tricks .com | Back To Top |