Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Ujumbe wa Viongozi 21 wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Chama cha kikomonisti cha China ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa na pia Kamati Kuu ya Chama cha Kikoministi cha China CCP Bw. Liu Yunshan hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema Tanzania na Bara zima la Afrika Limekuwa na kasi ya maendeleo kutokana na nguvu za msukumo wa China licha ya Baadhi ya Mataifa ya Magharibi kulalamikia hatua hiyo ya china.
Alisema uwekezaji wa Makampuni ya China katika Miradi ya Kiuchumi hasa yale ya Maadini, Viwanda na Miundo mbinu ya Mawasiliano imeweza kusaidia mapato ya Taifa na kuongeza ajira kwa Wazalendo waliowengi hasa Vijana
Amesema kuwa Wenzetu wa Magharibi wanalalamikia kasi ya China Kuvamia Bara la Afrika kiuchumi lakini wamesahau kuwa China ni mshirika wa Bara hili tokea Nchi zetu zinadai Uhuru kutoka kwa hao wanaomlalamikia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo kwamba Zanzibar bado inahitaji nguvu za Jamuhuri ya Watu wa China katika kuimarisha Uchumi wake.
Balozi Seif alisema Wawekezaji na Makampuni ya China yana nafasi nzuri wa kuwekeza miradi yao Zanzibar hasa katika Sekta ya Utalii na Viwanda.
Aliipongeza China kwa Juhudi za kutoa Taaluma kwa watendaji mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo wale wa Sekta inayondelea kuimarishwa hivi sasa kwa ajili ya utoaji ajira ya Uvuvi.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa na pia Kamati kuu cha Chama cha Kikoministi cha China Bwana Liu Yunshan alimueleza Balozi Seif kwamba Nchi yake itaendelea kuunga mkono sekta za Uchumi na Maendeleo ya Tanzania na Zanzibar kwa jumla.
Bw. Liu alisema Makampuni mengi yameonyesha hamu ya kuendelea kuwekeza katika maeneo ya Umeme, Madini na Viwanda kufuatia rasilmali iliyopo Nchini Tanzania.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu cha Chama Cha Kikomonisti cha China (CCP) amesisitiza kwamba uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya China na Tanzania na Zanzibar unastahiki kuimarishwa zaidi.
Ujumbe huyo wa Viongozi 21 kutoka Jamuhuri ya Watu wa China upo Nchini Tanzania kwa ziara rasmi na tayari umeshakukutana kwa mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Kutembelea sekta za Kiuchumi.
Ujmbe huo ambao ulifanya ziara ya siku moja Zanzibar ulitarajiwa kuondoka leo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR






0 comments:
Post a Comment