Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) akizindua mojawapo ya kisima cha maji katika kijiji cha Kibata Kata ya Mtamaa A, kisima hicho kimechimbwa kwa thamani ya zadia ya shilingi milioni 21.
MO akipampu maji katika kijiji cha Kibata tayari kwa matumizi.
Mbunge MO akimtwisha maji mama mmoja mkazi wa kijiji hicho Mariam Juma mara baada ya kuzindua kisima hicho wakati wa ziara yake jimboni humo.
MO akiangalia ujenzi wa msikiti katika Kata ya Utemini ambao unatarajiwa kuwa wa ghorofa moja, katika kuunga mkoni juhudi za waum,ini hao amechangia kiasi cha shilingi milioni 10.
MO akiwagawia nguo baadhi ya watoto wasiokuwa na uwezo wa kijiji cha Itisi mara baada ya kufanya kazi ya akuzindua mradi wa maji safi na salama.
Mbunge MO akizungumza na waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa miradi ya maji katika vijiji 17 ambavyo vimeanza kuchimbwa mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 awamu ya pili, miradi hiyo imemgharimu zaidi ya nusu bilioni.






0 comments:
Post a Comment